Wednesday 13 February 2013

WAZIRI MKUU MK PINDA AWASHAWISHI WADAU KUWAJALI WATOTO




WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wadau mbalimbali yakiwemo mashirika kujikita katika kuyasaidia makundi yasiyojiweza wakiwamo watoto waishio mazingira magumu.

Aliyasema hayo juzi alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha SOS Children’s Village kilichopo eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru, mkoani Arusha na kujionea hali halisi ya kituo hicho. Alisema kumekuwapo na ongezeko kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaotokea katika maeneo mbalimbali hali ambayo imekuwa ikisababishwa na walezi ama wazazi wao kutokana na migogoro katika familia na kusababisha watoto wengi kutoroka nyumbani na kuishia mitaani.

Alisema kutokana na hali hiyo kumekuwapo na idadi kubwa ya watoto ambao wamekuwa wakilelewa katika vituo mbalimbali na kupatiwa huduma za kijamii. Pinda katika kuona umuhimu wa kituo hicho pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili alichangia Sh60 milioni kusaidia kutatua changamoto mbalimbali kituoni hapo.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja ambaye alimuunga mkono waziri mkuu kwa kuchangia Sh10 milioni.

No comments:

Post a Comment