Sunday 1 May 2011

KESI YA HAPPY FREDDY wa MIKOCHENI IHARAKISHIWE HUKUMU

HAPPY FREDDY (28), mkazi wa Mikocheni, anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kusababisha kwa makusudi kifo cha mtoto wa kiume wa siku moja kwa kumdumbukiza chooni. Kamanda mkoa-polisi wa Kinondoni Bw. Charles Kenyela ametaarifu kuwa, tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8 mchana huko maeneo ya Mikocheni 'A'.

Kenyela amesema kuwa, taarifa hiyo iliifikia polisi baada ya wifi wa mtuhumiwa aitwae Shadya Ally (18) kupeleka taarifa kituo cha polisi Osterbay. Amesema mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake Mikocheni alianza kusikia uchungu wa kuashiria kutaka kujifungua na alimuomba wifi yake huyo amsindikize hospitali .

Kamanda akiendelea kutoa taarifa hiyo alisema kuwa, walianza safari ya kumpeleka hospitali lakini wakiwa njiani ghafla mtuhumiwa ambae ni ‘Happy’ alimwambia wifi yake huyo kuwa anajisikia haja na alishuka eneo hilo kwenda chooni kujisaidia na Shadya alimsubiri nje.

Amesema ghafla Shadya akiwa nje alisikia sauti ya mtoto ikilia kutoka chooni humo na aliamua kuingia na kukuta kichanga cha jinsia ya kiume kikiwa kimeegeshwa pembezoni mwa tundu la choo na kutoelewa ilikuwaje.

Kenyela alisema” wifi mtu aliamua kuwasha tochi ya simu yake ya mkononi na alimwona vizuri mtoto huyo na ghafla mtuhumiwa alikisukumiza kichanga hicho ndani ya tundu la choo kwa mguu wake na kwa madai kuwa alikuwa ameharibika. Hivyo kufuatia tukio hilo Shadya aliomba msaada kwa majirani na kutoa taarifa kituo cha polisi kuomba kuopolewa kwa kichanga hicho na walifanikiwa kuokoa mwili huo kwa kushirikiana na polisi ukiwa tayari mfu.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na polisi kufuatiwa tukio hilo. watotoz.blogspot.com inapendekeza kuwa mashauri ya mashtaka kama haya ya wazi, yanayowahusu watoto wasioweza kujitetea,  yasiigharimu serikali uchumi mkubwa kufikia hukumu. HAYA NI MAUAJI YA TAIFA.
                                          Habari za awali na Pilly Kigome wa Dar es salaam.

1 comment:

  1. watu wengi wanatumia advantage ya watoto kutokuwa na nguvu za maumbile au kauli dhidi ya watesi wao zaidi ya kujitetea kwa maumivu na uchungu, kuwanyanyasa vibaya. Taasisi za serikali na asasi za kujitegemea lazima zitilie mkazo usalama wa watoto.
    Mwikwabe

    ReplyDelete